28 Julai 2019 - 07:36
Mahathir Muhammad: Israel ni chimbuko kuu la ugaidi duniani

Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa Malaysia amekosoa vikali njama zinazoendeshwa katika majukwaa ya kimataifa kwa ajili ya kulifanya suala la kughusubiwa ardhi za Palestina lisahauliwe na kusema kwamba, kuasisiwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndio sababu kuu ya ugaidi duniani.

(ABNA24.com) Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa Malaysia amekosoa vikali njama zinazoendeshwa katika majukwaa ya kimataifa kwa ajili ya kulifanya suala la kughusubiwa ardhi za Palestina lisahauliwe na kusema kwamba, kuasisiwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndio sababu kuu ya ugaidi duniani.

Dakta Mahathir Muhammad amesisitiza udharura wa kuhuishwa kadhia ya Palestina na kusema kwamba, kuna harakati inafanyika ya kulifanya suala la Palestina lisahauliwe kabisa kama vile hakuna kilichotokea; na hakuzungumziwi au kuashiriwi kabisa ya kuwa vipi Wapalestina waliporwa ardhi yao ili kuundwa dola la Kizayuni.

Waziri Mkuu wa Malaysia amesema kuhusiana na mpango uliojaa njama wa Marekani wa 'Muamala wa Karne' kwamba, mpango huo ni sehemu inayohusiana na utatuzi wa matatizo yao; yaani wahusika kuhalalisha hatua na ukiukaji wao wa sheria dhidi ya Wapalestina.

Kadhalika Mahathir Muhammad Waziri Mkuu wa Malaysia amesisitiza kwamba, mpango wa Marekani wa 'Muamala wa Karne' unakiuka bayana sheria na kanuni za kimataifa.

Mpango wa Marekani wa "Muamala wa Karne" umedharau haki za mamilioni ya wakimbizi wa Palestina, unahimiza kupokonywa silaha wanamapambano wa Palestina, unataka kuundwe nchi ya Palestina isiyo na jeshi na pia unahimiza kupokonywa Wapalestina na Waislamu mji wao mtakatifu wa Quds na kupewa Wazayuni, yote hayo ni miongoni mwa sababu za kufeli mpango huo wa Marekani hata kabla ya kuanza kutekelezwa.



/129